Sababu ya kifo cha kijamii
Mtukufu Mtume (saw) ametaja sababu ya kifo cha jamii. Jamii hufariki wakati majukumu ya kuamrisha mema na kukataza maovu hayatekelezwi. Wakati kila mtu anahusika tu na masilahi yake binafsi na hajali kuhusu wengine na jamii, basi jukumu hili halitekelezwi na jamii inakuwa mfu. Wakati wengi wa watu wanapoombwa kuwashawishi wengine kuelekea kwenye mema na kukataza maovu, wanajibu “hili litanisaidia nini?” na halikadhalika wakati wanapoambiwa kuhusu maovu ambayo wao wenyewe wamejitumbukiza kwayo, wanasema “Hili litakusaidia nini?” Wakati kaulimbiu kama hizo zinapoibuliwa na watu kuombwa kujitokeza ili kutekeleza majukumu yao ili kuondoa maovu katika jamii ikiwa ni pamoja na maovu yao wenyewe, wao wanachukulia kuwakataza wengine kufanya maovu ni kuingilia mambo ya mtu binafsi, na maelekezo ya kuacha maovu yao wenyewe huchukuliwa kama kuingiliwa na wengine katika maisha yao binafsi, hivyo mambo yanapokuwa hivyo basi kuwa na hakika kwamba hawa sio wanadamu wanaoishi bali minyoo ya jamii. Wakati kaulimbiu kama hiyo inapokuwa ndio mtazamo na mwelekeo wa jamii basi jamii kama hiyo huchukuliwa kama mfu na watu wanaoishi katika jamii hizi wenye mitazamo kama hiyo ni kama minyoo katika mzoga.
Kuamrisha mema ni jina la kukanusha mantiki hizi. Ina maana ninajali mambo ya wengine na wengine wanajali mambo yangu, ina maana ninayo haki ya kuwaamrisha wengine wajiepushe na maovu na wengine halikadhalika wanayo haki ya kuniamrisha nijiepushe na maovu. Wakati wengine wakifanya maovu na makosa lazima niwazuie, na wakati nikifanya maovu wengine lazima wanizuie, huu ni wakati ambapo jamii zilizokufa zinahuika. Lakini kwa ujumla leo wakati tukimuona kijana akifanya kitendo cha uovu tunageuza nyuso zetu mbali na yeye huku tukisema “Hilo linanihusu nini?” Na kama kuna minyoo katika mzoga, kutakuwa na mnyoo mmoja mkubwa ambao utakuwa kiongozi wa minyoo hii, kwa sababu mkubwa na kiongozi wa minyoo vilevile atakuwa ni mnyoo. Mtu ambaye ana nguvu zaidi ya kukwangua minofu na kunywa usaha zaidi na damu kutoka kwa jamii; kwa misingi ya mamlaka yake anakuwa kiongozi wa minyoo hii. Anajitokeza nje na bendera yake na kutangaza kwamba kama ukandamizaji unatokea Palestina msijihusishe na kama watu wanauawa kikatili huko Iraq usijihusishe, unatakiwa kujali tu kuhusu mambo yako mwenyewe binafsi katika maisha. Sauti kama hizo zinatoka tu kutoka kwenye jamii zilizokufa na sio kutoka katika jamii zilizo hai, kwa sababu katika jamii zilizo hai Kuamrisha Mema na Kukataza Maovu hufanyika. Jamii zilizo hai ni zile ambazo Mtukufu Mtume (saw) alisema:
“Mtu anayeamka asubuhi na akawa hajali kuhusu mambo ya Waislamu wengine, huyo sio Mwislamu.”
Mwislamu wa kweli ni yule ambaye anaamka asubuhi na kutafuta kuhusu hali ya ndugu zake katika ulimwengu wa Kiislamu, Waislamu wa jumuiya hii na miji yao. Lakini kama anaamka bila kujali na kwenda zake kazini na kurudi jioni baada ya kukwangua minofu ya mzoga, na mfalme wa minyoo hii anamwambia kwamba usijali kuhusu mambo ya Waislamu wengine, basi huyo ni miongoni mwa minyoo ya jamii zilizokufa. Hii ni kanuni ambayo wakati jamii zinapokufa basi viongozi wao vilevile ni minyoo mibaya mno. Basi tutegemee nini kutoka kwa viongozi kama hawa? Minyoo hii ya mizoga hutafuta haki kutoka kwa kiongozi wao ambaye naye vilevile ni mnyoo mkubwa. Je, hili ni jukumu letu kuomba haki kutoka kwa mnyoo huyo mkubwa? Jukumu letu sio hili bali ni kuelewa jinsi gani jamii hii iliyokufa ilivyojitokeza na kuwepo, jinsi gani huu mnyoo mkubwa ulivyojitolea na kuwa na madaraka; umepata madaraka kwa sababu ya kufa kwa jamii hiyo. Kwa hiyo, jukumu letu na wajibu wetu ni kuihuisha jamii hii iliyokufa